February 2, 2019


SIMBA leo watakuwa Uwanjani kumenyana na Al Ahly ya Misri, huku aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Shiza Kichuya akitarajiwa kuivaa Al Ahly kwa staili yake kabisa.

Kichuya ambaye siku chache baada ya Simba kutua Misri aliuzwa kwenda timu ya Ligi Daraja la Pili nchini humo ijulikanayo kwa jina la Pharco, jumanne ijayo anatarajiwa kuwa uwanjani akiwa na kikosi cha ENPPI kitakachocheza dhidi ya Al Ahly.

Pharco baada ya kumsajili Kichuya kwa mkataba wa miaka miwili imempeleka kwa mkopo kwenye kikosi kinachoshiriki Ligi Kuu ya Misri cha ENPPI  ambacho jumanne ya wiki ijayo kitacheza na Al Ahly ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu nchini humo.

Kutokana na usajili huo Simba ilimuondoa Kichuya kwenye orodha ya wachezaji ambao leo jumamosi watacheza na Al Ahly mchezo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, ENPPI inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 20 kwenye msimamo.

Kutoka Championi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic