February 23, 2019


Kocha Mkuu wa klabu ya Zesco United inayoshiriki Ligi Kuu Zambia, George Lwandamina, ameonesha nia ya kumtaka kiungo wa Yanga, Mkongomani, Papy Tshishimbi. Imeelezwa.

Lwandamina ambaye aliwahi kuifundisha Yanga na kisha baadaye kuondoka kimyakimya kutokana na klabu kupitia wakati mgumu wa kifedha, ameonesha kuvutiwa na kiungo huyo.

Taarifa imeeleza kuwa tayari kumekuwa na mipango inayoongozwa na mabosi wa Zesco kufanya namna ya kumalizana na mchezaji huyo ambaye ameanza kurudi katika kiwango chake.

Habari za ndani zinasema pia katika mchezo uliopita dhidi ya Simba, ulikuwa moja ya mechi ambazo mabosi hao waliutumia kumfuatilia vizuri zaidi na wakiamini anaweza kuwa na mchango mkubwa ndani ya timu.

Wakati Zesco wakiwania saini ya Tshishimbi, kikosi cha Yanga kipo Lindi hivi sasa tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Namungo FC katika kombe la FA.

3 COMMENTS:

  1. Huyu Tshishimbi niliwahi kusikia kuwa Simba pia walikuwa wanaitaka saini yake

    ReplyDelete
    Replies
    1. mwenye kisu kikali ndio atakeyukula nyama anayoitaka kula.

      Delete
  2. Kuna timu zenye uwezo zinangojea kinyanganyiro cha wachezaji bora

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic