February 24, 2019


Watani wa Jadi Yanga na Simba walikutana Jumamosi ya tarehe 16, Februari kwenye Uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ukichezeshwa na mwamuzi Hance Mabena.  

Kwa mujibu wa waamuzi wastaafu Osman Kazi na Manyama Bwire, mwamuzi huyo alichezesha vizuri kwa sehemu kubwa licha ya mapungufu machache ya kibinadamu ikiwemo kuinyima Simba penati kufuatia tukio lililotokea dakika ya 49 kati ya Abdallah Shaibu na John Bocco. 

4 COMMENTS:

  1. Hiyo TFF imejaaa siasa hadi kichefuchefu yaani hovyo kabisa. Ninja huyo huyo ndie aliempiga mtu kiwiko hivi karibuni na hakuna hatua yoyote iliochukuliwa zidi yake hadi hivi sasa. Katika mechi ya Simba ninja huyo huyo alicheza fouls nyingi za hatari ikiwemo ile aliekwenda kumrukia mchezaji wa Simba okwi nadhani na kama sikosei na kama mchezaji yule wa Simba asingejitahidi kumuepuka ninja basi tungekuwa tunazungumza mengine mabaya zaidi kwa mchezaji wa Simba hivi sasa yaani hatarii. Waamuzi wanatakiwa kuwa makini na kazi yao lakini wanatakiwa kuwa makini zaidi kwenye mechi ya Simba kwani ni timu yenye wachezaji wanaocheza kwa kasi au tuseme ni timu yenye fowadi hatari zaidi kwenye ligi kuuu na mara nyingi hutokezea kufanyiwa fouls nyingi za ajabu ajabu na hata marefaree wanaonekana kushindwa kuendana na kasi yao ya mchezo kitu ambacho utaona mara nyingi Simba inakoseshwa haki zake nyingi za msingi kwenye mechi zao,mfano kukataliwa magoli yao mengi ya wazi, kunyimwa penalt nyingi za wazi kabisa yaani utahangaa. Kumbuka Simba inacheza soka la kiwango cha timu kumi sita bora barani Africa wakati kati ya waamuzi wa ligi kuu sidhani kama kuna hata mmoja anaechezesha mashindano hayo. Huwezi kuichukulia poa timu ambayo ina uwezo wa kwenda kuifunga timu kama Alahly tena mwenye mashindano muhimu kama klabu bingwa barani Africa, watanzania mara nyingi huwa tunashindwa kujua ubora wa vitu vyetu na kuvienzi kwa stahiki inayoakikana. Kuna sababu nyingi za marefa ligi kuu kuwalinda wachezaji wa Simba kutofanyiwa fouls za kijinga sio kuwapendelea lakini wachezaji wa Simba wana majukumu mengine makubwa zaidi ya kuliwakilisha Taifa. Mchezaji kuumia mchezoni ni jambo la kawaida ila tahadhari lazima zilichukuliwe kwa kuwadhibiti na kutoa adhabu za mfano bila ya kuchelewa kwa wale wachezaji wanaojiuhusisha na fouls za hatari.

    ReplyDelete
  2. cha muhimu Simba alipata point tatu!Hivi Yanga wangenyimwa penalti ingekuwaje. Ninja anathema za dhahiri kuchelewesha kutoa haki ni sawa na kuendeleza dhuruma

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mna ubora gani wakati mechi mbili goli kumi bora mkae kimya tu.Viroporopo nyie kama msemaji wenu.

      Delete
  3. Cha ajabu Yanga wanalialia hovyo wanaonewa na marefa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic