March 24, 2019


KIKOSI Cha Stars kimetakata leo baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Uganda mchezo unaochezwa Uwanja wa Taifa ambao mashabiki waliojitokeza ni kama wote.

Mabao ya Stars yalianza kuwekwa kimiani na Simon Msuva dakika ya 21 akimalizia pasi ya John Bocco bao ambalo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili mapinduzi yalikuwa makubwa ambapo Erasto Nyoni alifunga bao dakika ya 51 akifunga kwa mkwaju wa penalti.

Dakika ya 57 Agrey Morris alifunga bao la tatu akimalizia pasi ya Bocco hivyo zimebaki sekunde kadhaa kufuzu hatua hiyo kwani matokeo ya Lesotho na CapeVerde ngoma droo.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic