March 12, 2019



BEKI mwenye rasta kichwani ambazo wengi huita kiduku anayekipiga KMC, Ally Ally 'Mwarabu' amesema kuwa haikuwa dhamira yake kujifunga mble ya wapinzani wake Yanga katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara.

Ally Ally alijifunga katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na nahodha wa Yanga Ibrahim Ajibu.

Bao lake lilikuwa la ushindi kwani lilidumu mpaka dakika 90 na kuifanya Yanga kubeba pointi tatu.

"Unajua watu wanashindwa kuelewa kwamba mpira mimi ni kazi yangu na uwezo nilioonyesha kwenye mchezo wetu ghafla wanausahau kwa kuwa nimejifunga hiyo sio sawa kwani haikuwa dhamira yangu.

"Mpira unamambo mengi na ndio maana hata umbo lake ni la duara ikiwa ina maana kwamba una uwezo wa kuzunguka na kudunda, bado nina nafasi ya kuitumikia timu yangu, bado nina pambana kuwa bora, imani yangu nitakuwa bora zaidi," amesema Ally.

KMC wanapoteza pointi zote sita msimu huu mbele ya Yanga baada ya mchezo wa kwanza kufungwa dakika za lala salama bao 1-0 na mchezo wao wa Juzi kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

7 COMMENTS:

  1. Mara moja inaweza kuwa bahati mbaya. Lakini mara 3 mfululizo inatia mashaka
    .Halafu mchezaji huyo huyo na timu pinzani hiyo hiyo.
    Ndio maana watu hawakuzungumza mechi ya kwanza alipojifunga dhidi ya Stendi na Yanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acheni uboya, amejifunga mara mbili hiyo ya tatu mnaipata wapi? Kuna no 5 asiyefanya faulo?

      Delete
  2. Mara ya tatu inayozungumzwa ni kufanya faulo ya makusudi karibu sana na goli tena ikiwa bado dakika 1.
    Watu wanachotilia shaka ni kwamba nini Owe beki yule yule kwa timu ile ile?
    Lazima watu watilie shaka .

    ReplyDelete
  3. Wanamtetea ni hao anaowanufaisha.Haiwezekani iwe ni yeye tu kila mechi. There is something fishy.

    ReplyDelete
  4. Kwenye mpira linawezekana..wanaomlaumu ndio wasiojua mpira.jamaa alikaza sana alikua man of the match kama sio kujifunga

    ReplyDelete
  5. Bukaba kafungisha goli mbili Soura mbona hamuongei? Kapiga kichwa kwa adui mkapigwa la Kwanzaa. Kasababisha Penati mkapigwa la pili nae kachukua mlungula?

    ReplyDelete
  6. Bukaba kafanya kosa mechi moja .Huyu beki kaza Tomi zake mechi tatu. Hakuna cha kuficha hajahongwa lakini anafanya makusudi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic