April 17, 2019


MCHEZO wa kesho kati ya Ndanda FC ya Mtwara na Azam FC unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa kutokana na Ndanda FC Kupigia hesabu kuwa kwenye 10 ya msimamo.

Ndanda FC ambayo imejikusanyia pointi 40 endapo itashinda mchezo wa leo itajihakikishia nafasi ya kuwa ndani ya 10 bora TPL.

Kikosi cha Azam bado kimejikita namba mbili kwani endapo watajikusanyia pointi tatu watafikisha pointi 69.

Azam FC wataingia uwanja wa Nangwanda Sijaona wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wao wa kwanza mbele ya Ndanda kwa mabao 3-0 uliochezwa uwanja wa Chamazi.

Tayari kikosi kimewasili Mtwara na kufanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kutafuta pointi tatu kesho.

Azam FC ipo nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 31 imejikusanyia pointi 66 huku Ndanda ikiwa imecheza michezo 11 imejikuanyia pointi 40.


2 COMMENTS:

  1. TFF na waamuzi pia mnajenga imani kwa watanzania kuwa mnawaonea Yanga kwa kukataa magoli yao....ligi ya mwaka huu tutajionea mengi....nadhani katika ligi zote hii ya mwaka huu imetia fora!...kwa madudu....Simba kucheza mechi 7 ndani ya siku 17...hata Patrick Aussems amelizungumzia hili...kwakweli tunapoelekea kama nchi si pazuri....si ajabu hata Serengeti Boys kutolewa....yaani laana inaitafuna TFF.....

    ReplyDelete
  2. hapa ni ndanda na azam yanga inatoka wapi tena jamani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic