May 8, 2019


JURGEN Klopp, Meneja wa Liverpool amesema kuwa alikuwa kwenye hali ya ajabu baada ya wachezaji wake kushinda dhidi ya Barcelona mabao 4-0 kwenye mchezo wao wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa uwanja wa Anfield na kujikuta akitokwa na machozi.
Liverpool inatinga hatua ya fainali kwa jumla ya ushindi wa mabao 4-3 baada ya mchezo wa kwanza kupoteza wakiwa ugenini kwa kufungwa mabao 3-0 na wao wakashinda mabao 4-0, mabao yaliyofungwa na Georginio Wijnaldum na Divock Origi.
Sasa wanasubiri kucheza fainali na mshindi wa mchezo kati ya Ajax ama Tottenham .
"Kama ingekuwa ni kuichanganua timu yangu kwa matokeo ilyopata moyo wangu ulikuwa unanisumbua kama mjinga fulani hivi ningeshindwa kutoa tathmini, dunia nzima ingejua kwamba mimi ni mjinga.
"Nina furaha kupita kiasi kupenya hatua hii ngumu na yenye ushindani kwangu, mchezo wote mwanzo mwisho ulikuwa ni mgumu usioelezeka, kuna vitu vingi duniani vya muhimu, niliwaambia wachezaji kushinda ni jambo rahisi ila ugumu upo kuzuia kushindwa kufungwa hapo ndipo hofu ilipojificha, ukichanganya na kutoamini pamoja na furaha unapata vitu ya ajabu ambavyo sijawahi kuvipata.
"Awali niliwaambia wachezaji itakuwa ngumu kwangu kupata matokeo, lakini kwa kuwa nafikiria juu yenu nina amini tunaweza kupata matokeo ila mwisho wa siku tumeshinda siamini kama tumeshinda," amesema Klopp.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic