May 9, 2019


Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo amewasili Moshi na kuungana na mamia ya waombolezaji kumsindikiza mzee wetu, Dkt. Reginald Mengi katika makazi yake ya milele leo Mei 9, 2019.

“Mzee Mengi alikuwa smart na simple, aliamini katika kuwekeza na kusaidia wasiokuwa nacho.
Alikuwa na nidhamu kubwa ya fedha, ndio maana alifika hapo na kupata mafanikio ambayo Taifa linaumia kwa kuondoka kwake leo.


“Jiulize ni vijana wangapi amewapandikiza hasira ya kuyatafuta mafanikio yao? Ni akina mama, vijana na watu wenye ulemavu wangapi ambao amewasaidia mzee Mengi? Alikuwa na moyo wa pekee!

“Nimejifunza mengi kutoka kwake. Mimi ninamuita #Championi. Alinyoosha njia ya vijana wengi kuthubutu na kujikwamua katika wimbi la umaskini. Safari umeimaliza, tangulia kiongozi wangu,” amesema Shigongo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic