May 8, 2019


TUKIO lililotikisa ulimwengu wa mastaa mwishoni mwa wiki iliyopita lilikuwa la ujio wa mwanamama Zarina Hassan ‘Zari’ kutoka Afrika Kusini ambaye mbali na mambo mengine aliyoyafanya, ameonesha jeuri ya kugoma katukatu kwenda kumsalimia mama mkwe wake, Sanura Kassim ‘Sandra’ kule Madale jijini Dar. 

Zari ambaye ni mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alitua Bongo Ijumaa iliyopita kwa shughuli za kijamii akiwa ni balozi wa Pampers za Softcare ambapo Team Zari walifika kwenye mapokezi yake kiasi cha kuwashangaza wengi.

Akiwa Bongo, Zari ambaye yuko kwenye vita baridi na Diamond, alitikisa mitaa ya Temeke pale alipotembelea katika Hospitali ya Mbagala ambapo mbali na kukutana na mashabiki wake, alitoa misaada mbalimbali kwa akinamama na watoto wenye uhitaji.

Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wake akiwa Mbagala, mwandishi wetu alipata fursa ya kufanya naye mahojiano ambapo katika maelezo yake alionesha kajeuri flani alipotajiwa suala la kwenda ukweni (Madale anakoishi Mama Diamond).

Alisema licha ya kwamba alikuwa ‘akiiva’ na mama mkwe wake huyo, hana mpango wa kwenda kumuona kule Madale huku akisindikiza na maneno ya nyodo kidogo kwamba, hana alichosahau kule.

“Niende kule kufanya nini sasa, kwani kuna kitu gani nimesahau? Siwezi kwenda Madale,” alisema Zari. Alipoulizwa kitendo cha mama Diamond kuwaposti mara kwa mara wajukuu zake hasa Tiffah kuwa kinaonesha amewamiss sana, Zari alisema:

“Sawa yeye awaposti tu, si ni wajukuu zake? Kwani kuna tatizo gani jamani, ila tu mimi siwezi kwenda kule Madale, siwezi.” Akizungumza mbele ya umati uliofurika kumsikiliza kwenye hospitali ya Mbagala, Zari alisema kuwa, amependa alivyopokelewa na kwamba yeye ataendelea kuwa wifi na shemeji wa Watanzania milele.

“Jamani mimi si mnajua nimezaa na kaka yenu, hivyo uwifi haufi, yaani nitakuwa wifi yenu forever, ndiyo maana ilikuwa lazima mnipokee vizuri na kwa kweli najisikia niko nyumbani,” alisema Zari na kuwaacha wanawake wengi waliokuwa eneo hilo wakimshangilia.

AIBUA MJADALA…

Kitendo chake cha kugomea kwenda Madale kimeonesha kuwakera baadhi ya watu ambao walisema kwa kuwa ametibuana na Diamond, angeonesha busara ya kwenda kumuona mama mkwe wake.

“Hii ni kuonesha jeuri kwa wakwe, Zari kazaa na Diamond na kweli wametibuana lakini kwa kuwa amefika Bongo, ingekuwa jambo jema kwenda kusalimia tu, angefanya hivyo ningemuona ni mtu kati ya watu,” alisema Zuleha Kassim wa Kinondoni jijini Dar. Naye Johnson Sumeer alisema: “Mimi sijui mahusiano yao kwa sasa yakoje lakini kiukweli kabisa alitakiwa kwenda Madale, sasa kama amegoma, ni yeye na maamuzi yake.”

TUJIKUMBUSHE KIDOGO

Zari ametua Bongo ikiwa ni siku chache zimepita tangu atoke kwenye kurushiana maneno makali na mzazi mwenzake, Diamond huku tuhuma nzito zikiwa ni kuchepuka enzi walipokuwa kwenye uhusiano. Hata hivyo, mbali na kuzinguana huko, wadau wengi walitarajia kuwa, Zari akitua Bongo atakwenda Madale, jambo ambalo aliligomea kwa sababu alizozijua mwenyewe

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic