June 20, 2019





Baada ya ukimya wa muda mrefu, hatimaye leo uongozi wa klabu ya Yanga umetoa msimamo wake kuhusiana na kiungo Ibrahim Ajibu Migomba.

Yanga imesema mkataba wake na Ajibu unaisha mwishoni mwa mwezi huu. Tayari wamemka Ajibu nafasi ya kuamua kama atasajili au la.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amesema tayari wameamuambia Ajibu kama anataka kubaki wanamhitaji lakini kama anataka kuondoka, wanamtakia kila la kheri.

"Tumemueleza nia yetu, kama anataka kubaki tunamsubiri kwa ajili ya kusaini lakini kama anataka kuondoka, basi tunamtakia kila la kheri," alisema.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwamba tayari Ajibu ameshamalizana na Simba ambayo ni timu yake ya zamani.




4 COMMENTS:

  1. Ebu tusijidhalilishe kupindukia mipaka
    tumwachilie inmekuwa kama tunambembeleza mtoto mchanga alale ingelikuwa anatutaka angekuja zamani mbona Kakolanya tulimwacha bila ya ubishi

    ReplyDelete
  2. Yanga imeshasajili viungo wengi sana.. Mini tena kubembeleza huyo mtu.! Acheni kumpaiza, wacha aende akakae benchi simba atajuta. Yanga mnabembeleza na usajili wote tuliofanya huu! Upumbavu then utoto.

    ReplyDelete
  3. Kiongozi Yanga, hivi kweli mnambembeleza Ajibu hadi leo? Tumwache aende zake. Huyu keshaamua.

    ReplyDelete
  4. Let him go where he wants, wapo wachezaji wazur pia japo ametusaidia sana msimu uliopita, ninaiman hatoacha pengo lisilozibika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic