IMEVUJA!! KABWILI ALISHAPATA OFA MACEDONIA AKILIPIWA KILA KITU, MPAKA SASA YUPO MORO
Imeripotiwa kuwa hivi karibuni ilisema kuwa klabu ya FK Renova ya Macedonia barani ulaya ilimpa ofa golikipa wa klabu ya Yanga, Ramadhani Kabwili ya kwenda kufanya majaribio ya wiki mbili.
Ofa hiyo ilitakiwa kuanza kwa majaribio June 24 na ikielezwa kuwa klabu hiyo itamgharamikia nauli ya ndege, chakula na malazi kwa wiki zote mbili ambazo atakuwa huko.
Licha ya ofa hiyo kutumwa, mpaka sasa Kabwili yupo Tanzania akiwa kambini Morogoro na klabu ya Yanga.
Haijajulikana mpaka sasa hatma ya suala lake limekaaje ingawa katika orodha ya majina ya Yanga yaliyopelekwa CAF jina lake halipo.
Ikumbukwe mkataba wa Kabwili na Yanga mpaka sasa umeshamalizika na yupo huru kuelekea pengine kusaka maisha.








Mkataba umeisha halafu moro anafanya nini? Lazima ujue kuwa Kabwili ni goalkeeper wa U20 Yanga. Ila alipandishwa kutokana na upungufu wa makipa, hivyo ukiwauliza Yanga au Kabwili watakupa majibu badala ya kukaa unatunga story chumbani unajifanya ni habari.
ReplyDeleteSasa km mchezaji wa under 20 timu ya wakubwa alikuwa anafanya nini? Na pia akiwa under 20 ina maana hana mkataba?
DeleteInatakiwa tujiridhishe kwanza kama ofa ilikuja kweli
ReplyDeleteNYIE WAANDISHI MBONA MNAKUA KAMA WAPIGA RAMLI
ReplyDeleteUnder 20!!!! Under 20!!!+
ReplyDeleteRashid Juma sisi tumempa mkataba na jina limeenda. Tusidharauliane bwana, ukipandishwa lazima usaini, hakuna mchezaji asiye na mkataba anayeruhusiwa kucheza ligi.
Au Mimi ndio sielewi?????
Ukanjanja fc wameanza tena
ReplyDeleteJamaa anadanganya sana Hadi kero.
ReplyDelete