ELIAS Maguli
huenda akatua nchini Kenya kusakata soka la kulipwa iwapo atakubali masharti ya
mabosi wa timu mpya inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya msimu ujao.
Imeelezwa kuwa Maguli ambaye ni mshambuliaji huru baada ya kuachana
na timu yake ya KMC ameingia kwenye anga za timu ya Gor Mahia ambayo inaendelea
kusuka kikosi chake.
“Kama
ambavyo wameanza na mchezaji kutoka Singida United, David Kissu sasa mpango
uliopo ni kumpata mshambuliaji ambaye hatakuwa wa gharama kubwa zaidi kwani
mambo mengi hayajawa sawa, na anayetajwa ni Maguli,” kilieleza chanzo hicho.
Maguli amesema kuwa mchezaji kazi yake kubwa ni kucheza hivyo hana tatizo na uwezo wake ni suala la muda tu kujua hatma yake.








0 COMMENTS:
Post a Comment