July 12, 2019


Mshambuliaji wa zamani wa Simba na baadaye Azam FC, Ramadhan Singano, amejiunga na TP Mazembe ya Congo.

Singano ambaye aliwahi kung'ara zaidi wakati akiwa Simba na baadaye kutimkia Azam FC, amefikia makubaliano na miamba hao wa Afrika kwa kuingia nao mkataba.



Singano amemwaga wino Mazembe akiwa na bosi wa klabu hiyo, Moise Katumbi na sasa atakuwa na kikosi hicho msimu ujao wa ligi.

Mchezaji huyo ambaye alibatizwa jina la Messi wakati akiichezea Simba alishindwana na Azam juu ya mkataba mpya baada ya msimu huu kumalizika.

4 COMMENTS:

  1. Akiwa na katumbi au picha ya moses katumbi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ha Ha Ha waandishi wa habari wa Bongo ni tia maji sana. Eti akiwa na katumbi wakati ni picha tu.

      Delete
  2. Acheni ushabiki maandazi, huyu ni mchezaji wa Azam. Kama ulitaka kuihusisha Simba ungesema mchezaji wa Zamani wa Simba. Hakukuwa na sababu, hivi wachezaji wote wanaosajiliwa huwa mnataja club zao zote walizopitia?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lakini pia sio mchezaji wa azam kwa sababu amemaliza mkataba na amejiunga akiwa mchezaji huru. Kwa hiyo ilikuwa kusema mchezaji wa zamani wa simba na azam.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic