July 12, 2019


IMEBAINIKA kuwa wakati Simba ikitarajiwa kuondoka kwenda Afrika Kusini kuweka kambi Jumatatu ijayo, klabu kibao za Sauz zimeomba kucheza mechi za kirafiki na Simba itakapokuwa huko.

Msimu uliopita, Simba ilifanya vyema kwenye michuano ya kimataifa na hata kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ndiyo maana timu nyingi zimevutika kujipima na Simba.

Simba itaanza kambi yake huko Sauz kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo michuano yote hiyo itaanza Agosti, mwaka huu.

Awali, Simba ilipanga kuweka kambi yake nchini Marekani lakini ilibadili mipango kutokana na hali ya hewa ya joto na kuhamia kwenye baridi ambako ni Sauz.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amethibitisha kuwa klabu nyingi za Sauz zinaomba kucheza mechi na Simba itakapokuwa huko.

Magori alisema kuwa wanasubiri wakifika kule ndipo watafanya maamuzi kuona ni klabu gani ambazo watadili nazo.

“Tunaenda kuweka kambi Sauz lakini pia tuna mpango wa kucheza mechi za kirafiki kwa ajili ya kujipima lakini mpaka sasa sijui tutacheza na timu ipi, sababu klabu tu kubwa za pale Sauz kila mmoja anataka kucheza mechi na sisi lakini hatujui mpaka sasa tutacheza na yupi.

“Lakini tukikaa na kutulia wakati tunaendelea na maandalizi huku, ndipo tutafanya maamuzi na kufahamu tutacheza na timu ipi, ila ufahamu tu kila timu inataka kujipima na Simba kutokana na hatua ambayo tulipiga kwenye msimu uliopita kimataifa,” alisema Magori. Hii itakuwa mara ya pili kwa Simba kuwahi kuweka kambi yake Afrika Kusini.

3 COMMENTS:

  1. Licha ya kufanya vizuri klabu bingwa Adrica vile vile baadhi ya wachezaji wa Simba kufanya vyema Afcon kumewashtua wengi na kumeiongozea Simba kitu fulani kikubwa na kuthaminika zaidi ndani na nje ya Africa. Na Simba wanatakiwa kufahamu hivyo kuwa klabu yao imepiga hatua ila la kuomba huu usajili mpya uwe bora zaidi ili wapige hatua zaidi ya walipofika.

    ReplyDelete
  2. Kabwili kaenda Ulaya ligi kuu,Ninja kauzwa kwenda Ulaya ligi kuu now anapelekwa kwa mkopo Marekani mshhara milioni 46 Kwa wiki!

    Ajibu akiwa Yanga alisumbuliwa sana Na TP Mazembe

    Kabwili naye kwenda Ulaya time nzuri tu!

    Sasa mbona kimataifa anacheza Simba lakini wachezaji wanaouzwa Ulaya ni wa Yanga.

    Kuna siri gani hapo?Nisaidieni wadau!

    ReplyDelete
  3. Mkomola naye kauzwa Ulaya!Pana mini,mbona simba waliojitangaza kimataifa wachezaji wao hawanunuliwi Ulaya!

    Salehe naomba majibu,Yanga wananini?Kuna Siri Gani?
    Halafu baada ya kuja Zahera naona wachezaji Yanga wanatoka sana hiyo Feitoto amefuatwa sana na hadi timu za ligi kuu England labda hawakusaini tu lakini walishaweka nia baadaye labda wakapata mbadala wana nini Yanga?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic