WACHEZAJI
wengi kwa sasa wanachekelea kusaini kandarasi ya miaka mitatu ama miwili kwenye
vikosi vipya hili ni jambo jema lakini je wanaangalia mbele ama macho kwenye noti?
Naona kila
mmoja anafurahi kuanza changamoto mpya mwisho wa siku anapotea na kusahaulika
kabisa kwenye ramani ya mpira.
Wachezaji
wanapaswa wawe na maamuzi magumu na sahihi ifike wakati watazame namna bora
itakayokuza viwango vyao kwanza kabla ya kukimbilia pesa ambazo zinawafanya
wafurahi kwa muda.
Furaha ya
mchezaji ambayo anaipata kwa kujiunga na timu itakayompa fedha huwa ni ya muda
mfupi baada ya msimu kuisha ndoto zake zinayeyuka kabisa.
Ukweli ni
kwamba wakati huu wa usajili ni muhimu kwa wachezji kujiuliza mara mbili
wanakwenda kucheza timu gani na wanagombania namba na nani?
Endapo
atajiuliza maswali haya itakuwa rahisi kwake kutoa maamuzi sahihi
yatakayomfanya aamue kusaini ama kubaki kwenye timu yake ambayo anaitumikia
kwa sasa.
Kama
mchezaji atafurahia dau alilowekewa mezani ilihali hana nafasi ya kucheza ni
bora aachane na hilo dili kwani litakuja kumgharimu baadaye.
Kama
atakomaa ili ajiunge na timu ambayo ina wachezaji wa kutosha gharama ya furaha
ya muda atailipa baadaye atakapokuwa anasugua benchi na kukumbuka kule
alikotoka.
Muda wa
furaha kwa wachezaji ambao wana uwezo wa kawaida huwa wa muda lakini muda wa
majuto huwa ni mkubwa na wa kudumu.
Nina mifano
ya wachezaji wengi ambao ni marafiki zangu pia awali walikuwa wanafurahia
kusaini kwenye timu walizozipenda mwisho wa siku wakapoteza furaha yao kwa
kukosa namba.
Wapo ambao
walikumbuka namna walivyokuwa wanapata nafasi kwenye timu zao za zamani ila
mwisho wa siku wakawa wameshapoteza dira.
Ukiachana na
hao wapo wale ambao walikuwa na rekodi nzuri walipotoka timu zao za awali ila
walipojiunga na timu nyingine walipoteana kabisa.
Ni wakati wa
wachezaji kutazama timu anayokwenda kucheza na kuangalia nafasi yake kama
ataona itakuwa ngumu kushindani ni kheri aache kwanza.
Siku zote
riziki ni kama ajali huja bila taarifa endapo mchezaji ataamua kulazimisha
mambo matokeo yake yatakuwa yenye maumivu kwake.
Itakuwa
busara kwa wachezaji kufanya uchunguzi mdogo kabla ya kukubali kujiunga na timu
ambayo imempa dili mezani asikimbilie kusaini.
Majuto siku
zote ni mjukuu kabla ya kufika muda wa majuto wakati huu uliopo ni sahihi kwa
mchezaji kusoma alama za nyakati kabla ya kukimbilia kujifunga na timu yake
mpya.
Wapo
wachezaji ambao sajili zao zilitikisa mwisho wa siku wakaishia kusugua benchi
na kukimbia timu kwa kukosa kile ambacho walikuwa wakikipata.
Wengine
walitolewa kwa mkopo ili kukuza viwango vyao na mwisho wa siku wakawa
wameshapoteza ujasiri wa kurejea kwenye ubora wao wakabaki kuwa wachezaji wa
kawaida ambao soko likawakataa mara ya pili.
Tatizo lipo hapa kwa vijana wetu wengi wa kitanzania ni kuendeleza furaha nakuwa starehe ndani ya kazi baada ya kubahatika kupata mkataba wenye maslahi mazuri na hicho ndicho kitu kinachowamaliza.vijana wetu wengi hawana eleimu ya kazi yao na miiko yake.Mpira kazi inayotegemea uwezo wa kujituma wa mtu binafsi kwanza na team work inafuta baadae.Mchezaji hawezi kubweteka kwakuwa tu amesajiliwa kwenye timu yenye wachezaji wazuri na yeye atakuwa mzuri hapana. Kwa mchezaji wa mpira mwenye malengo makubwa zaidi hasa vijana Tanzania bado hapajafikia kiwango cha kumfanya mchezaji abweteke na hela ya mkataba.
ReplyDelete