HITIMANA
Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa hana presha na vigogo wa Ligi Kuu
Bara akikutana nao lazima awape usumbufu na kupata matokeo.
Namungo FC
imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu na itakuwa miongoni mwa timu 20 ambazo
zitashiriki ligi inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 23.
Thiery amesema kuwa maandalizi ya mwisho kwa sasa yapo sawa wana
imani ya kufanya makubwa ligi ikianza.
“Tupo sawa
na kikosi chetu kina moto wa kutosha kabla ya ligi kuanza hivyo imani yetu ni
kufanya makubwa msimu utakapoanza hasa ukizingatia tumepambana kupanda daraja.
“Hatuna timu
ambayo tunaihofia kwenye ligi hata hao vigogo ambao ni Simba, Yanga, Azam na
timu nyingine zaidi ya kuziheshimu kwa kuwa tumezikuta ila tutakapokutana nao
uwanjani lazima tuonyeshe kuwa tupo tofauti,” amesema Thiery.
0 COMMENTS:
Post a Comment