August 10, 2019


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa nafasi bado ipo kwa timu hiyo kusonga mbele kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga leo imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Township Rollers mchezo uliochezwa uwanja Taifa.

Rollers walianza kuandika bao la kwanza dakika ya 7 kupitia kwa mshambuliaji wao Phenyo Seremeg kabla ya Patrick Sibomana kuweka usawa kwa mkwaju wa penalti dakika ya 87.

Zahera amesema:'Ilikuwa ni makosa yetu kushindwa kupata ushindi mapema kwani wachezaji niliwaambia kazi ya kwanza ni kushinda nyumbani kabla ya kuwafuata huko kwao.

"Kwenye michezo ya Ligi ya Mabingwa kitu cha muhimu ukiwa nyumbani ni kupata ushindi kabla ya kwenda kurudiana ila bado tuna nafasi kwa kuwa nasi tumefunga bao," amesema.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 nchini Botswana.

9 COMMENTS:

  1. Kwenda kushinda ugenini?Give me a break!Kwa mpira gani?

    ReplyDelete
  2. Shida bongo soka ni figisu tu. Uongozi unahangaia tamasha badala kambi na trial mech za kimaifa.

    ReplyDelete
  3. Ukipanda mbigili huwezi kuvuna mahindi.Safari umeishia hapo.

    ReplyDelete
  4. Nafasi bado Yanga wanayo tena sana ila tuwe wawazi na viongozi wa Yanga ndio walioizoiifisha Yanga kushindwa kufanya vizuri. Nina sababu tatu za msingi kwanini viongozi wa Yanga ndio walioizoifisha Yanga kushindwa kufanya vizuri kwenye mechi yake ya kwanza klabu bingwa Africa msimu huu kutofanya vizuri
    .
    (1) Viongozi wamezembea na wanaendelea kuzembea kulishughulikia suala la akina Yondani na wenzanke.Hili ni tatizo na unapozunguzia timu ina maana ni mfano wa mwili mzima wa mwanadamu kiungo kimoja kikiwa na matatizo basi mwili wote lazima utikisike.
    (1) Yanga walikuwa hawana sabau ya kukataa kwenda kushiriki sekafa kagame cup kule Rwanda na kukimbilia morogoro na kwenda kucheza mechi za kujipima nguvu na Moro kids. Yale mashindano kagame cup yakewajenga sana Yanga wala wasingepanick kwenda kuwachosha wachezaji wao dakika za mwisho kule Zanzibar.
    (3) viongozi wamemuachia Zahera kuchelewa kuja kujiunga na timu wakati timu ilikuwa ipo kwenye pre season kwa kiasi fulani inashangaza. Labda alikuwa na mgomo baridi lakini ni kama vile Zahera anajiamulia kila kitu apendavyo ndani ya Yanga yaani ZAHERA yupo juu kuliko Yanga ni hatari sana kwa maendeleo ya timu.

    ReplyDelete
  5. Mechi za zanzibar hazikua na umuhim sana.....halaf ttz jingin n kwamb h mechi y marudio 90% huwa referee wanachaguliwa kutok zone zao huko kusini nasi figis za namn h bado hatuja ziweza

    ReplyDelete
  6. Mwenyekiti wa Yanga Dk. Msolwa anasema wanaenda kuweka kambi Moshi halafu unajipima nguvu na timu za Polisi yaani hamko serious kwakweli nilifikiri wanasema wataenda kuweka kambi South Africa kwa wiki 1....Mimi naona kulikuwa na makosa kuingiza timu 4....nyingine zinaishia njiani ikiwemo Yanga....unashindwa kutumia nguvu na hali na mali kushinda nyumbani kwako unategemea miujiza ugenini....lakini hili halinishangazi kwasababu dalili zilijionyesha mapema tu kwanza kocha kuchelewa kujiunga na timu, uongozi kutoiweka timu kambi iliyobora nje ya nchi baadhi ya wachezaji kutoingia kambini na kufikiria wiki ya mwananchi kuliko mechi za CAF CL....matokeo yake timu ina asilimia 95% kutolewa raundi ya 1 ya CAF CL

    ReplyDelete
  7. Hata tatizo la baadhi ya wachezaji muhimu wa Yanga kushindwa kutumika kwa kuchelewa leseni zao ni uzembe wa viongozi wa Yanga. Huyo Shikalo hakutajwa leo kama anakuja kucheza Yanga vipi vibali vya CAF vichelewe? Mpira sio blah blah za siasa mpira ni kuwajibika. Wanayanga wajuwe tu sio Simba wanaoleta figisu ndani ya timu yao ila bado viongozi wao hawajajua nini wanatakiwa kufanya ili kukizi thamani ya Yanga.

    ReplyDelete
  8. Lawama haisaidii kitu wandugu...tuungane tuwe wamoja timu sio mbaya hata kidogo..kama wametoa draw kwetu nasi tuna uwezo wa kushinda kwao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic