LEO Yanga itakuwa uwanja wa Taifa kumenyana na Township Rolers huku KMC wao wakiwa nchini Rwanda wakimenyana na AS Kigali na Simba nao Msumbiji wakimenyana na UD Songo.
Mechi zote ni muhimu kwa timu zetu kufanya vema na kupata matokeo hasa ukizingatia kwamba ni mechi za mtoano.
Yanga ambao wao watakuwa nyumbani ni wakati wa mashabiki kujitokeza kwa wingi Taifa kuwapa sapoti.
Shabiki ni mchezaji wa 12 hivyo uwepo wake ndani ya uwanja kutaongeza nguvu ya kupambana.
Simba ambao wao wapo ugenini wana kazi ngumu na kubwa kwa ajli ya Taifa wanapaswa waonyeshe ukomavu wao leo.
KMC wapo kwenye mchezo wao wa kwanza leo kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho wana uwezo wa kuonyesha kile ambacho mashabiki wanakihitaji.
Si kingine ni ushindi tu na kila kitu kinawezekana kwa timu ambazo zitakuwa uwanjani kwa wachezaji kujituma kutafuta matokeo mwanzo mwisho.
Watanzania wanaungana na timu zote bila kuisahau Azam FC ambayo kesho itakuwa ugenini kuvaana na Fasili Kenema nchini Ethiopia.
Mchezo wa kwanza unatoa picha ya kule ambako tunakataka kwenda na ni muhimu kumaliza kazi mapema ili kupunguza presha mchezo wa marudio.
Michezo yote ya marudio inatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 ni muda wa kuchanga karata kupata matokeo chanya.
Saleh Jembe, inaungana na watanzania wote kuwaombea kila la kheri wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa.
Kazi kubwa ambayo mnayo kwa sasa wawakilishi wa Taifa ni kupambana kwa ajili ya Taifa kila kitu kinawezekana.
Pia hakuna timu ambayo itakutana na timu nyepesi zote ni ngumu na kubwa ndio maana zinashiriki michuano hiyo ila cha msingi ni kujua kwamba zinafungika.
0 COMMENTS:
Post a Comment