KIUNGO wa Liverpool, Alex Oxlade-Chamberlain amedai kuwa Mohamed Salah sio mchoyo wa pasi kama ambavyo wengi wanamfikiria.
Mzozo wa ishu ya uchoyo uliibuka baina ya Salah na mshikaji wake wa karibu Sadio Mane kwenye mchezo dhidi ya Burney na Liverpool ilishinda mabao 3-0.
"Huwezi kutegemea kila wakati Salah ana mpira basi atoe pasi.Hiyo ni staili yake ya uchezaji wake na ndio maana anafunga mabao mengi yanayotusaidia kushinda mechi, hivyo haina maana kwamba ni lazima atoo pasi akiwa ndani ya eneo la 18.".
Kwa sasa Mane na Salah wote ndani ya Liverpool wamepachika jumla ya mabao manne na msimu uliopita walitwaa kiatu cha dhahabu baada ya kufunga jumla ya mabao 22.
0 COMMENTS:
Post a Comment