FUNGU la pili la wachezaji watano wa Azam FC waliokuwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', limeshatia timu nchini Zimbabwe kwa ajili ya maandalizi ya kuivaa Triangle United.
Hivyo kwa sasa jeshi la Azam FC lipo kamili gado baada ya msafara ya kwanza kuongozwa na Idd Cheche kutangulia kuweka mazingira sawa.
Fungu hilo limeungana na wachezaji wengine ambao walitangulia awali kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa Septemba 28.
Wachezaji hao walibaki Bongo kuitumikia timu ya Taifa iliyocheza na Sudan uwanja wa Taifa mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Chan.
Wachezaji hao ni Frank Domayo 'Chumvi', Mudathir Yahya na Shaaban Chilunda, ambao wameanza mazoezi huku Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije, akiwapumzisha kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' na winga Idd Seleman 'Nado'.
0 COMMENTS:
Post a Comment