UONGOZI wa
KMC umesema kuwa kwa sasa hesabu zao ni kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo
wao wa tatu utakaochezwa leo uwanja wa Azam Complex.
KMC iliyo
chini ya Kocha Mkuu, Jackson Mayanja imepoteza michezo yake miwili ilianza
mbele ya Azam FC ilifungwa bao 1-0 uwanja wa Uhuru na ilipoteza kwa kufungwa
mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, Mkwakwani.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa kwa sasa
tayari makosa ya awali yamefanyiwa kazi wana imani ya kupata pointi tatu mbele
ya Namungo.
“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Namungo, michezo iliyopita
hatukufanya vizuri kwa sasa tunatazama namna tutakavyorejea kwenye ubora wetu.
“Tunahitaji
pointi tatu kwa wapinzani wetu na tunawaheshimu pia kwani wao hawajapoteza
mchezo hata mmoja ila hilo halitupi taabu tutakuwa nyumbani tutapambana
kushinda mashabiki watupe sapoti,” amesema Binde.
0 COMMENTS:
Post a Comment