Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems juzi asubuhi alitua katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, akiwa na mkewe kwa ajili ya kula bata baada ya kupata mapumziko ya muda mfupi.
Aussems atakuwa katika hifadhi hiyo mpaka kesho ambapo atapata nafasi ya kujionea vivutio mbalimbali wakiwemo wanyama.
Habari za kuaminika ambazo Championi Jumatano, limezipata kutoka ndani ya Simba zimedai kuwa Aussems ameenda Serengeti kwa ajili ya mapumizo ya siku mbili kwa kuwa wachezaji wengi wapo na timu zao za taifa kwa sasa.
“Kocha ameondoka leo (jana), kwenda Serengeti kwa ajili ya mapumziko na atarejea Dar es Salaam, Alhamisi mchana. “Jamaa anapapenda sana Serengeti na hii ni mara yake ya pili kwenda huko kila anapopata mapumziko ya muda mfupi,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Hata hivyo, Aussems alipotafutwa kwa njia ya simu ili aweze kuthibitisha juu ya hilo alisema kwa kifupi: “Nipo nje ya Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko.”
CHANZO: CHAMPIONI
Kula bata kocha wetu sio huyo mvaa kaptura
ReplyDeleteZahera naona anamezea mate, nenda basi na wewe hata ngurdoto
ReplyDeleteloh,jamani nalionea huruma hili livaa kaptura,litakula mihogo mibichi mpaka basi,nyamipensi vinjunga
ReplyDeleteKweli kuna tofauti huko na wanyama wa mjini.
ReplyDeleteKweli kuna tofauti huko na wanyama wa mjini.
ReplyDeletena mwaka huu lazma tukufukuzishe kazi
ReplyDelete