UONGOZI wa Yanga umewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi Septemba14 ili kuwapa sapoti wachezaji wakipambana kwenye mchezo wa hatua ya kwanza na wa kimataifa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa kwa sasa kikosi kipo vema na kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo huo wa kimataifa.
"Kwa sasa tupo Mwanza na tunaendelea kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Zesco, tunatambua kwamba haitakuwa kazi nyepesi ila tupo tayari.
"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti na kuwashangilia wachezaji ni jambo la busara na muhimu kwani timu ni yetu sote na lengo letu ni kufanya vizuri," amesema.







This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteHOJA NI MOJA TU KUUJAZA UWANJA.....UMOJA WA WANANCHI NA MASHABIKI NA WAPENZI WA YANGA NDIYO SILAHA YA USHINDI
ReplyDeleteHata mjaze uwanja kichapo lazima. Nitawashangalia Zesco mwanzo mwisho.Uzalendo wa kinafiki siuwezi.
ReplyDeleteHela yako,uende usende no sawa tuu,washingilie.mwanzo mwisho timu ya wananchi ushindi ni lazima
ReplyDeleteUta2kuta tena shirikisho
ReplyDelete