AHUKUMIWA MIAKA 14 KWA KUMUUA RADIO
MTUHUMIWA Godfrey Wamala amekutwa na hatia ya kumuua msanii Moses Sekibogo (Mowzey Radio) bila ya kukusudia.
Hukumu hiyo imesomwa licha ya Mwanamuziki huyo kufariki katika ghasia zilizotokea sehemu ya starehe.
Kesi ilikuwa ikiendeshwa na Jaji Jane Abodo katika Mahakama Kuu Entebbe ambapo Jaji amesema kuwa Godfrey Wamala atatumikia miaka 13, miezi 3 na siku 4 baada ya kukaa mahabusu kwa mwaka 1 katika Gereza la Kigo.
Imeelezwa kuwa, siku ya tukio, Godfrey Wamala alimpiga Radio hadi akapoteza fahamu na kulazwa Hospitali ya Case alikofariki.
Adhabu kiduchu sana
ReplyDelete