November 1, 2019


JUMA Mwambusi, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa wachezaji wake walikosa utulivu kuifunga timu ya Alliance jana kwenye mchezo wa ligi uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mbeya City jana ikiwa ugenini kwenye uwanja wa Nyamagana ilipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana na wachezaji wawili wa timu ya Alliance FC kuonyeshwa kadi nyekundu.

Mwambusi amesema: "Wachezaji wangu walishindwa kuwa makini katika kumalizia nafasi ambazo walizitengeneza kwani uwezo wa kushinda ulikuwa kwetu.

"Kilichobaki kwa sasa ni kufanya maboresho kwa makosa ambayo tumeyafanya jambo litakalotufanya tufanye vizuri kwenye michezo mingine inayofuata, mashabiki watupe sapoti," amesema.

Mbeya City imecheza jumla ya mechi nane ambazo ni sawa na dakika 720 imejikusanyia pointi nane ikiwa nafasi ya 16 kenye msimamo wa ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic