MARTIAL SASA KUFUNGA KILA MECHI
Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amesema kuwa mshambuliaji wake Anthony Martial anatakiwa kukua na kuanza kufunga mfululizo.
Martial amekuwa mmoja kati ya washambuliaji mahiri kwenye timu hiyo kwa msimu wa tatu sasa, lakini hana muendelezo kwenye kiwango chake.
Kocha huyo amesema kwa sasa mchezaji huyo anatakiwa kuhakikisha anajituma kwenye kila mchezo ili awe mchezaji wa msaada kwenye timu hiyo.
“Ukiwa mshambuliaji, unatakiwa kuhakikisha unafunga mabao kwenye kila mchezo ambao unacheza.
“Martial amekuwa sasa na hata tabia yake mazoezini inaonyesha kuwa ni mchezaji mkubwa ambaye alisajiliwa kwa ajili ya kuisaidia Man United, nafi kiri anatakiwa kufanya hivyo sasa.
“Kwa sasa ni mchezaji mwenye furaha na kila siku amekuwa akionyesha kuwa yeye ni bora na hakika ni mchezaji anayestahili kuheshimika, lakini lazima afahamu kuwa anatakiwa kufunga kwenye kila mchezo,” alisema kocha huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment