Maamuzi hayo yamekuja mara baada ya Mtibwa kupendekeza mechi zao za nyumbani zichezewe katika uwanja huo badala ya Jamhuri Morogoro ambao ulikuwa ukiwapa gharama kubwa.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru, amesema bodi imeridhia kuwapa uwanja huo na sasa mechi zao zote za nyumbani zitachezewa katika uwanja huo.
"Ni rasmi sasa bodi ya ligi imetukabidhi uwanja wa CCM Gairo kuutumia kwa ajili ya mechi zetu za nyumbani.
"Tumepokea vizuri maamuzi haya sababu itarahisisha gharama za kwenda Jamhuri Morogoro ambako ilikuwa ikitufanya tutumie kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya timu."
Ikumbukwe kabla ya ligi kuanza, bodi iliufungia uwanja wa Manungu ambao Mtibwa walikuwa wakiutumia miaka yote kwa mechi za nyumbani kutokana na kukosa hadhi.








Tuulizane..CCM Gairo unafaa kuchezea mechi za ligi????TFF mpooooo
ReplyDelete