November 1, 2019


Wachezaji wa Barcelona wako tayari kuchelewa kulipwa mshahara ikiwa hatua hiyo itasaidia klabu klabu hiyo kumsajili tena mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar msimu wa joto, anasema beki, Gerard Pique.

Barcelona ilifanya kila ''liwezekanalo katika uwezo wake'' kumsajili nyota huyo wa kimataifa lakini juhudi hizo ziligonga mwamba.

Neymar aliondoka Barcelona na kujiunga na Paris St-Germain kwa ada ya kuvunja rekodi duniani ya euro milioni 222 sawa na (£200m) mwaka 2017.

Pique alisema wachezaji wenzake waliiambia klabu hiyo kuwa wako tayari kuchelewa kulipwa mshahara ili kuisadia kufikia kanuni ya klabu ya malipo sawa ya wachezaji.

"Tuko tayari kandarasi zetu zifanyiwe marekebisho," Pique alikimbia kituo cha radio cha Cadena Ser cha Uhispania.

"Hutuna mpango wa kuchanga pesa, lakini tutarahisisha mambo kwa kuruhusu baadhi ya malipo kutekelezwa katika mwaka wa pili au watatu badala ya mwaka wa kwanza."

Barcelona ilitumia zaidi ya £200m msimu wa joto, katika usajili wa wachezaji kama Frenkie de Jong, kiungo wa kati kutoka Ajax na Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid.

Kanuni ya malipo sawa ya wachezaji, ambayo inazuia vilabu kutumia fedha kuliko uwezo wao, inasadikiwa kuwa moja ya suala ambalo Barcelona inatakiwa kushughulikia kabla ya kumsaini Neymar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic