November 9, 2019


BAADA ya kikosi cha Singida United kushindwa kupata ushindi wowote katika michezo 11 waliyocheza mpaka sasa msimu wa Ligi Kuu Bara, hali inazidi kuwa mbaya zaidi kwa kikosi hiko. 

Singida United, juzi Jumatano ilikubali kichapo cha mabao 5-1 kutoka kwa Lipuli FC hali ambayo imedhihirisha kikosi hiko kuwa katika hali ngumu kutokana na idadi hiyo ya mabao kuwa kubwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United, Festo Sanga alisema japokuwa timu yake imeanza ligi kwa matokeo mabovu lakini haimfanyi yeye na benchi la ufundi kukata tamaa ya kushuka daraja kwani wanazidi kujipanga kwa ajili ya kuanza kufanya vizuri.

“Hakuna mtu anayependa matokeo mabaya, sisi tunafanya vibaya kwa sasa lakini hatukubali kuendelea na hali hii, tumejipanga kuhakikisha tunaanza kufanya vizuri kwa ajili kuepuka masuala ya kushuka daraja,” alisema Sanga.

Naye, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema: “Tunapata tabu sana kwa sasa na tunatambua kwamba mashabiki wanaumia, ni suala la muda tu kurejea kwenye ushindani, kwa sasa tunaomba sapoti tu hamna namna.”

Singida United kwa sasa ina pointi 4 ambazo imezipata baada ya kutoa sare michezo minne, ikifungwa michezo saba kati ya 11 sawa na dakika 990 huku ikishika mkia katika msimamo wa ligi kuu.

Ikumbukwe timu hiyo ilikuwa inafadhiliwa na Mbunge ambaye pia ni mwanachama wa Yanga, Mwigulu Nchemba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic