November 1, 2019


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa una imani ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa marudio wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids utakaochezwa Novemba 3 nchini Misri.

Yanga ilipoteza mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba kwa kufungwa mabao 2-1 jambo lililoongeza mzigo kwa Yanga ambao wanatakiwa kuifunga Pyramids mabao 2-0 ili kusonga mbele.

Fredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa kikosi kina morali kubwa na makosa waliyoyafanya yanafanyiwa kazi kwa ukaribu.

"Kupoteza mchezo wa kwanza haikuwa hesabu zetu kwa kuwa makosa tumeshayatambua tunayafanyia kazi na tutapambana kupata ushindi.

"Wao wametufunga nyumbani basi nasi tuna nafasi ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa marudio mashabiki watupe sapoti," amesema.

Yanga imewafuata wapinzani wao tayari kwa ajili ya mchezo huo wa marudio utakaopigwa nchini Misri.

2 COMMENTS:

  1. Yanga haijawahi hata kuifunga timu ya kiarabu tofauti ya magori mawili yani kama 2-0,3-1,4-2 zaidi ya 1-0 au 2-1 wakicheza hapa tanzania alafu waende kupindua meza tushawazoea mmewaotea Rollers mkaona mmeitoa zinga la timu 6-0 zinawahusu

    ReplyDelete
  2. Tangu lini waarabu wakawa na meza ambayo yanga wanaenda kupindua . Ushahidi wa kauli hii nenda kwa Bakhresa pamoja na uwezo wake kifedha ukikuta dinning room yake kuna meza nitumie namba yako nikurushie jero

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic