KIKOSI cha Yanga leo kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Iringa United kwenye mchezo wa hatua ya 62 Kombe la Shirikisho uliochezwa uwanja wa Uhuru
Dakika ya saba Yanga ilipata bao la kuongoza lililopachikwa kwa kichwa na nahodha Papy Tshishimbi aliyemalizia pasi ya Patrick Sibomana.
Yanga ilitumia dakika mbili kupachika bao la pili kupitia kwa Patrick Sibomana aliyefunga bao hilo akiwa ndani ya 18 baada ya mabeki wa Iringa United kujichanganya na lile la tatu likipachikwa na beki kisiki Lamine Moro dakika ya 38 kwa kichwa akimalizia pasi ya Patrick Sibomana.
Dakika ya 69 David Molinga alipachika bao la nne akimalizia pasi ya Patrick Sibomana akiwa ndani ya 18 na kuongeza mzigo kwa Iringa United ambayo ilishindwa kufurukuta mbele ya Yanga iliyokuwa na njaa ya kufunga mabao mengi.
Dakika ya 72 Adam Kiondo wa timu ya chini ya miaka 20 aliingia kwa Yanga akichukua nafasi ya Deus Kaseke.
Licha ya mpira kusimama kwa muda wa dakika tano baada ya nyuki kuvamia uwanja dakika ya 52 na kutulia mpaka dakika 56 bado Yanga ilizidi kukaza licha ya kuwan’gata baadhi ya wachezaji ikiwa ni pamoja na Ally Mtoni na mlinda mlango wa Yanga Farouk Shikalo.
Kwa ushindi huo napendekeza I kocha huyo wa sasa apewe nafasi kuendelea kuinoa Yanga ambae anaijuwa timu ndani nje badala ya kuleta mpya Kuanza kuvuruga mambo
ReplyDelete