Pamoja na Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, kulalamikia mwenendo wa ratiba, amesema ana uhakika mkubwa wa timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kutokana na mabadiliko makubwa yanayoonekana katika kikosi chake.
Luc alisema wana ratiba ngumu kwao kwa sababu wanacheza mechi zaidi ya tisa katika mwezi mmoja, hivyo watapambana kuhakikisha wanapata pointi kwenye kila mchezo ili kufikia malengo yao.
Alisema kutokana na ugumu wa ratiba yao na wachezaji kuchoka atahakikisha kikosi chake kitakuwa na mabadiliko ya mara kwa mara lengo likiwa ni kutafuta pointi muhimu ambazo zitawafanya kutwaa taji la ligi hiyo linaloshikiliwa na watani zao, Simba waliopo kileleni wakiwa na alama 53 baada ya mechi 21 ikiwa ni alama 15 zaidi ya Yanga yenye michezo miwili mkononi.
"Licha ya ratiba kuwa changamoto kwetu, kikubwa ambacho nakiona kwenye timu yangu imebadilika kwa kiwango kikubwa na kadiri siku zinavyo kwenda ndiyo inazidi kuwa bora, naamini nafasi ya ubingwa tunayo tena kubwa.








Mechi tisa katika mwezi!Mwambie kuna wakati mwaka jana Simba ilicheza mechi 10 katika wiki mbili..Aache malalamiko..Tena kwa kuwa Simba katika wiki chache zilizopita imekuwa ikicheza kila baada ya 72hrs..Basi tunaomba TFF itende haki kwa kuwapangia Yanga wamalize viporo vyao kwa mechi kila baada ya 72 hours..Ni muhimu anachokipata Simba na Yanga pia akipate...Ili hapo awali bingwa awe ni halali
ReplyDeleteMadawa anayotumia ni makali sana
ReplyDeleteMadawa anayotumia ni makali sana
ReplyDeleteUliona wapi ndani ya siku 14 timu ikacheza mechi 10 kama sio porojo porojo tu mnazotoa nyie mikia,tatizo lenu hamjui kutafsir lugha anayoongea kocha wa yanga
ReplyDelete