February 14, 2020


Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, amefunguka kuhusiana na suala la kuitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kutoa maneno ambayo si rafiki na yenye kashfa mitandaoni kwa TFF na ligi kwa ujumla.

Nugaz ameeleza kuwa yeye yupo tayari na ameeleza anasubiria barua maalum kutoka TFF ili aweze kuitia agizo hilo.

Kiongozi huyo ambaye hivi karibuni alitangazwa na Yanga kuwa Mhamasishaji, amesema atawajibika na hana mengi zaidi ya kueleza mpaka pale atakapokamilisha alichoitiwa katika Kamati hiyo ya Maadili.

Mbali na Nugaz, Msemaji wa klabu ya Simba naye ameitwa kwenda kunako kamati hiyo kujibu tuhuma zake kuandika maneno ya kashfa na yasiyo rafiki kwa taasisi hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic