February 29, 2020


TIMU ya Yanga leo imefuta bundi la sare iliyokuwa ikiwaandama kwa kushinda mbele ya Alliance FC mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Februari 29 Uwanja wa Taifa.

Ushindi huo uewafanya mashabiki kujawa na furaha na kusahau sare nne mfululizo kwa mwez Februari mbele ya Mbeya City, Prisons, Polisi Tanzania na Coastal Union.

Mabao yote ya Yanga yamepachikwa kimiani na nyota wao mpya aliyejiunga na timu hiyo akitokea Polisi Tanzania alikokuwa kwa mkopo akitokea Azam FC, Ditram Nchimbi.

Allingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Tariq Seif dakika ya 45 na alifunga mabao hayo dakika ya 48 kwa kichwa akimalizia pasi ya Bernard Morrison na dakika ya 78 baada ya mabeki wa Alliance kujichanganya.

Ushindi huo unaifanya Yanga kuongeza pointi tatu ila inabaki nafasi ya nne ikiwa na pointi 44.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic