USHINDI wa bao 1-0 walilopata Azam FC mbele ya JKT Tanzana limewapa matumaini Azam FC kuendelea kasi yake kufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Azam FC imecheza mechi 25 kwenye Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 48.
Vinara wa ligi ni Simba wakiwa na pointi 62 bada ya kucheza mechi 24 za ligi.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa ushindi huo umerudisha morali kwa wachezaji wataendelea kupambana kufikia malengo waliyojiwekea.
Kwakuwa na Yanga nao wana uhakika wa Kuutwaa ubingwa basi ni heri wagawane
ReplyDelete