March 24, 2020



BEKI wa klabu  ya Valencia, Alessandro Florenzi ametengwa kwa miezi miwili sasa baada ya kukutwa na maambukizi ya aina tofauti.

 Beki huyo awali alitengwa peke yake kwa mwezi mmoja baada ya kuugua tetekuwanga(Chikenpox) lakini sasa ametengwa kwa mwezi mmoja baada ya kupata maambukizi ya Virusi vya Corona.

 Mchezaji huyo alijiunga na Valencia kwa mkopo Januari mwaka huu akitokea katika klabu ya Roma.

Hivi karibuni alipimwa Virusi vya Corona  na akakutwa na virusi lakini alipojipima mwenyewe majibu yameonyesha kuwa hana maambukizi.

Florenzi baada ya kutengwa awali alikosa mechi dhidi ya Atletico Madrid, Atalanata na Real Sociedad, lakini baadaye alicheza dhidi ya Real Betis na alikaa benchi mechi dhidi ya Alaves na Atalanta.

Beki huyo kwa msimu huu amecheza dakika 160 tu kabla ya La Liga kupigwa stop kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic