March 25, 2020


DROO ya Kwanza ya Shindano la Jishindie Gari inayoendeshwa na Kampuni ya Global Group kupitia magazeti yake ya michezo ya Championi na Spoti Xtra imefanyika leo Jumatano, Machi 25, 2020, makao Makuu ya Group Group yaliopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam na washindi watatu kutoka mikoa mitatu tofauti wameibuka washindi kwenye droo hiyo.

Droo ya kwanza ilirushwa moja kwa moja na Global TV Online na ilishuhudiwa na Mkaguzi wa Masuala ya Michezo ya Bahati Nasibu, Elibariki Sengasenga.


 Washindi hao ni pamoja na Neema Chuma mkazi wa Kinyerezi ambaye alijishindia simu ya mkononi ambaye alisema kuwa anajivunia kuwa mwanafamilia ya michezo.

Swaleh Mohamed (27) mkazi wa Tanga na Yesse Daniel (27), mkazi wa Moshi alikamilisha idadi ya washindi watatu wa kwanza kwenye droo hiyo ambaye ni shabiki wa Simba wote walisema kuwa wanafurahi kushinda kutokana na kushiriki mara kwa mara na kuwashauri wasomaji kuendelea kushiriki Shindano hilo.


Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally Jembe amesema kuwa droo ya kwanza imefanyika kwa mafanikio chini ya msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Sengasenga na malengo makubwa ni kurejesha shukrani kwa wasomaji. 

“Tumeanza na droo ndogo na zawadi bado zinaendelea kwani hatubahatishi tunafanya kwa kushirikiana na wasimamizi wa Bahati Nasibu na kuponi zilizotumika leo zitaendelea kutumika kwenye droo ya pili na Ile kubwa pia zitatumika, wasomaji waendelee kujisomea ili kupata burudani na habari,” alisema.


Elibarik Sengasenga, Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania alisema kuwa anawapongeza washindi wote na Kampuni ya Global Group kwa kuanzisha shindano hilo.


JINSI YA KUSHIRIKI


Nunua Gazeti la Championi au Spoti Xtra, kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

JINSI YA KUTUMA


Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic