June 1, 2019

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa anaona ajabu kwa nini nyota wake watatu wa kikosi cha kwanza hawajaitwa timu ya Taifa itakayoshiriki michuano ya Afcon nchini Misri mwezi Juni mwaka huu.

Aussems amesema kuwa ni muda wa Taifa kutumia wachezaji wenye uzoefu wa mashindano ya kimataifa kwa kuwa wana changamoto mpya ambazo wamezipitia.

"Kwa Taifa ambalo linaingia kwenye michuano ya kimataifa kuna haja ya kuwatumia wachezaji wale ambao wameshiriki michuano ya kimataifa, vijana kama Ndemla,(Said), Rashid (Juma) Salamba (Adam) ni miongoni mwa wenye uzoefu wa kimataifa kwa kuwa wameshiriki michuano ya kimataifa na timu imefika hatua ya robo fainali.
"Uwepo wao ndani ya kikosi ungefanya kuwe na changamoto ya namba ila maamuzi ya mwalimu huwezi kumpangia kwa kuwa naye ana mtazamo wake," amesema Aussems.

8 COMMENTS:

  1. Wabongo bhana! Utafikiri tunaenda kucheza na Ndanda fc kule misri..

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa wachezaji wa simba wamepata uzoefu mkubwa nani bora sana kuliko timu yoyote nchini

    ReplyDelete
  3. Nadhani ufike wakati tuzungumze kimichezo bila U yanga na U simba wetu, Afcon sio kwa kupeleka watu kwa sababu ya ushabiki bali ushindani. Salamba, Juma wachukue nafasi ya nani stars iliyosheheni wachezaji wenye uwezo? Hivi kwa macho yetu hatujashuhudia Adam Salamba kiwango chake kushuka? Patrick Ausems yupo kisimba simba, amwache Amunike afanye kazi yake. Ni mwono wangu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sure....ili siamini kama hiyo ni kauli ya Ausems....Uchebe ni very professional huwa hawezi kuzungumzia maamuzi ya kocha mwenzie hususani wachezaji ambao yeye hajawaamini vya kutosha hata kwenye mechi za ligi

      Delete
  4. Ausems ameongelea experience ya wachezaji sasa unataka kile kikosi cha Eswatin ambacho hata Mkuu wa Nchi kilimchefua,elewa huyo ni kocha wa daraja la juu.

    ReplyDelete
  5. Sio Ausems hiyo stori imepikwa lazima tuwe tunajiongeza sio kushadidia tu.Ausems ni very profesional huwa hawezi kuzungumzia maamuzi ya kocha mwenzie....pia hawezi kupendekeza waitwe stars wachezaji ambao mwenyewe hajawatumia kwenye michuano ya kimataifa.Nikiwa shabiki wa simba nasema hao wote kwasasa hawana nafasi stars (....tuache unafiki mpira unachezwa hadharani).Huwezi kwenda afcon eti unamtegemea Rashid Juma, Ndemla, Boxer, Ajib, Shabalala, Sonso,Ninja etc....experience ni kitu mhimu sana.Ukimuacha Rashid hao wengine wana uzoefu wa kusafiri sio kucheza.Wachezaji wengi wanaocheza ligi ya ndani ukimwondoa Moris, Boco, Yondan wakitoka kwenda kwenye mechi za vilabu/Taifa stars nje ya Tz ambako hakuna mashabiki ni sifuri kabisa....ndio maana simba sasa wamejikita kusajili kwa kuzingatia experience na ubora ili kuepuka zahma iliyotukuta.

    ReplyDelete
  6. Kwa salamba hakuna hata ndemla hajampa mechi za kimataifa labda rashid juma

    ReplyDelete
  7. Sio kocha wa simba, hii imepikwa tu.. Uchebe kwanza anawatoa kwa mkopo wote hao walio tajwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic