March 30, 2020


BERNARD Morrison, Kiungo Mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kabla ya kutua Bongo alipata ofa nyingi Afrika Kusini pamoja na Ghana ambapo ndipo maskani yake ilipo.

 Morrison ni ingizo jipya ndani ya Yanga alisajiliwa akiwa mchezaji huru na miongoni mwa timu ambazo alizicheza ni pamoja na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

 "Nilikuwa na ofa nyigi mkononi kutoka timu mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile za nyumbani Ghana, Afrika Kusini na Ulaya ila zote niliamua kuziacha ili nije Bongo ambapo nipo kwa sasa kwa sababu nilipenda kupata changamoto mpya nje ya Afrika Kusini. 

"Mwanzo nilikuwa ninataka kwenda Afrika Kusini lakini nikaona ni bora nije hapa ndani ya Yanga ambapo nipo kwa sasa na maisha yanaendelea," amesema.


Morrison amecheza mechi 10 za Ligi Kuu Bara ndani ya Yanga ametupia mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao.

8 COMMENTS:

  1. Yaani amekacha kwenda Ulaya ili acheze Yanga???Ukiambiwa neno changanya na zako.

    ReplyDelete
  2. Kila siku lazima kuna habari za morrisson? What is soo special with him?

    ReplyDelete
  3. Ivi huyu morrison ana kitu gani cha ziada kinachopelekea mumuandike kila siku? Yaani kumfunga Simba kigoli kimoja tena cha kutenga ndio inapelekea mumvimbshe kichwa namna hii!! Acheni hizo jamani. Na Yanga angebahatika kuchukua ubingwa mbona tungekoma!!!

    ReplyDelete
  4. Huyo muongo , , halaf hii blog kwa sasa haina news kila cku habar hizohizo tu , ss hv Belarus ligi inaendelea ni bora mngekuwa mnatupa update za huko tu

    ReplyDelete
  5. Wewe mwandishi acha kuwachefua Wana mikia,unajua wengine wako majumbani wakijitibu korona

    ReplyDelete
  6. Hata kama ni mahaba kwa mtu haya yamezidi. Asubuhi, mchana jioni, morrisson. Hakuna wachezaji wengine mtuhabarishe?

    ReplyDelete
  7. Tuandikieni hata basi kina balama,juma Abdul niyonzima nao tujue kuwa wapo,sasa kila siku morisoni,Sina uhakika na jinsia ya mwandishi kama angekuwa mwanamke ningesema kamzimia ila cjui ke au me.kuna wachezaji wengi tunahitaj kujua habari zao,huyu tayr tumemjua tuleteeni mwingine jamani.

    ReplyDelete
  8. hatuna cha kuandika tumebaki kudanganyana.hii mambo ya hadithi njoo.....utamu kolea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic