NAMUNGO FC leo imeibana mbavu Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa kwa kulazimsiha sare ya kufungana bao 1-1.
Yanga ilianza kuinyoosha Namungo FC dk ya sita kupitia kwa Tariq Seif liliwapeleka Namungo vyumba vya mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili Namungo FC walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Bigirimana Blaise dakika ya 62.
Sare hiyo inaifanya Namungo kufikisha pointi 50 ikiwa nafasi ya nne huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 51.
Inaumiza na kutuvunja moyo na kuwapa vicheko wapinzani wetu na pia kuwaumiza wanaotowa hela Yao Bila ya kuona faida isipokuwa droo zisizokwisha. Tusikate tamaa tuendelee kupambana huko mbele tushinde zote zilizobakia. Wakubwa wakae na kujuwa kosa liko wapi
ReplyDeleteVyura vimekwisha na vimebakia kuropokwa eti bado hawajakata tamaa. Hah
ReplyDeleteUtopolo katika ubora wao
ReplyDeleteGONGOWAZI HOOOOO VYURA HAOOOO KANDAMBILI HAOOOOO KMC JUUUU NAMUNGO WAMEAMBULIA SARE HAOOOO KANDAMBILI HAOOOOO
ReplyDeleteVITENDO VYA VIONGOZI WA SERIKALI WENYE MAPENZI NA SIMBA
ReplyDeleteMbona watu wa Simba wamekasirika sana mpaka viongozi wa serikali (Waziri Mkuu-Namungo fc & Mkuu wa Mkoa Dsm-Simba&KmC) ambao hawapaswi kuegemea upande wowote wanaipania Yanga (utafikiri Yanga ni timu kutokea Kenya) na wanaonyesha mapenzi yao dhahiri na kwa uwazi hili si jambo zuri na linaweza kuleta mtafaruku na mgawanyiko katika jamii iliyo na umoja uliojengwa na waasisi wa Taifa hili...(Mwl. Nyerere, na Sheikh Karume). Mambo ya Mpira yasitugawe katika umoja wetu na Viongozi waliopewa dhamana ya utawala kwa wananchi....dini zetu, mapenzi yetu kwa timu za mpira yasitugawe!
sikatai kuhamasisha michezo katika jimbo lake la uchaguzi ila Waziri Mkuu anapotoa kauli yenye amri na maagizo yenye utashi binafsi kwa uongozi wa wilaya kumbuka timu pinzani na waamuzi hufikia kwenye mahoteli na guests zote hizo ziko wilayani kunaweza kukawa na shinikizo la hujuma kufanyika kwenye mchezo husika....hiyo ndiyo hoja yangu. Na pia pale Mkuu wa Mkoa anapoingilia katika kuitunza ahadi ya fedha timu moja iliyo katika Mkoa mmoja na timu pinzani, inaleta taswira ya upendeleo na inajenga imani ya chuki kwa timu nyingine....mapenzi binafsi ya viongozi wa serikali katika timu za mpira nasisitiza kwa mara nyingine yasitugawe na yasitutenganishe kwani huu umoja na mshikamano wa kitaifa na udugu ulioasisiwa na waasisi wa Taifa letu...mwalimu Nyerere na Sheikh Karume na muda mrefu.....(hata wao walikuwa na mapenzi ya timu za soka) lakini hawakuwahi kukandamiza timu nyingine!
Ni maoni yangu
Ahsanteni
Saleh jembe hvi anayebanwa mbavu ni mwenyeji au ni mgeni? Yanga anabanwaje mbavu wakati yuko ugenini? apo aliyebanwa mbavu ni mwenyeji ambae ni namungo na sio yanga, na goli lenyewe la namungo la offside wamepewa zawadi na lanzimeni labda kwa maelekezo maalum kama kawaida yao
ReplyDelete