May 4, 2020


BEKI Kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani ambaye aliwahi kuwa nahodha wa kikosi hicho inaelezwa kuwa miongoni mwa mabeki anaowakubali ndani ya Bongo ni pamoja na beki chipukizi anayekipiga ndani ya Mtibwa Sugar, Dickson Job.

Yondani anayevaa jezi namba tano mgongoni inaelezwa kuwa ameishauri Yanga kuinasa saini ya chipukizi huyo ili waungane ndani ya kikosi cha mabingwa wa kihistoria.

 "Miongoni mwa mabeki anaowakubali Yondani ni pamoja na yule Job anayecheza Mtibwa Sugar, huenda akaitwa mezani ili kuzungumza na Yanga juu ya yeye kutua Jangwani," ilieleza taarifa hiyo.

Job amesema:-" Sijazungumza na kiongozi yeyote wa timu ya Yanga kuhusu mkataba wangu ila kuna watu ambao sio viongozi wamekuwa wakinipigia simu kuuliza juu ya suala hili."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic