DR.Hassan Abbas,Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni. Sanaa na Michezo amesema kuwa kuanzia ligi itakapoanza mashabiki ni ruksa kwenda viwanjani lakini kwa kuzingatia muongozo ambao umetolewa na Serikali.
Awali baada ya Serikali kuruhusu kuanza kwa masuala ya michezo ifikapo Juni Mosi, ilitolewa taarifa kwamba mashabiki watakaoruhisiwa kwenda uwanjani ni 20 ambapo kila timu ingetoa mashabiki 10 na hii ilitokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Leo, Mei 31, kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari, uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dr. Abbas amesema: "Serikali imeridhia mashabiki watakaotaka kwenda uwanjani wanaruhusiwa kwenda kama utaratibu ulivyokuwa awali, kabla ya Virusi vya Corona, pia nyingine zitaonyeshwa ‘live’ kama kawaida, lakini lazima wafuate muongozo na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
“ Kila uwanja, shabiki atapimwa joto na kwa upande wa mechi kubwa ambazo zitahusisha mashabiki wengi na kuleta changamoto kwa upande wa mita moja, maelezo ni kuwa wataingia nusu ya wanaotakiwa kuingia uwanjani.
"Serikali inahitaji kuona furaha inarudi kwa mashabiki na watanzania ndio maana haikuzuia masuala ya kiuchumi, shughuli zinaendelea kama kawaida lakini ni lazima kuzingatia utaratibu unaowekwa na muongozo kwa yule atakayekiuka adhabu kali juu yake zitahusika kwani Serikali inajali," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment