IMEELEZWA kuwa fainali ya mchezo wa Kombe la FA inayotarajiwa kuchezwa Agosti Mosi, Uwanja wa Wembley itahudhuriwa na idadi ya mashabiki 20,000.
Kwa sasa viongozi wanapambana kuona namna gani wanaweza kupata kibali hicho ili kupata kibali cha kuwa na mashabiki katika fainali hizo kutokana na janga la Virusi vya Corona kutibua mipango mingi katika soka.
Ripoti zinaeleza kuwa moja ya kigezo ambacho kinatakiwa ili kupata kibali hicho ni pamoja na kupungua kwa maambukizi ya Virusi vya Corona mpaka kufikia asilimia 0.5 kwa muda ambao fainali itakaribia kupigwa.
Hesabu kubwa ni kuwagawa mashabiki 20,000, ambapo kila upande utakuwa na mashabiki 10,000. Msimu huu zimebaki timu nane ndani ya FA ambapo Leicester City wao watamenyana na Chelsea, Newcastle United dhidi ya Manchester City, Sheffield United itamenyana na Arsenal huku Norwich itakutana na Manchester United hatua ya robo fainali.
Kwa sasa imekuwa ngumu pia kwa mashabiki wa Premier kuona uhondo wa mechi zinazotarajiwa kuanza kurindima Juni 17 kwa mechi zilizobaki ila kuna matumaini makubwa kwenye fainali ya FA mambo iwapo mambo yatabadilika.
0 COMMENTS:
Post a Comment