May 30, 2020


IMEELEZWA kuwa uongozi wa Simba umeanza kufanya mchakato wa kuwarejesha wachezaji wake watatu ambao wamekwama kutokana na mipaka yao kufungwa.

Taarifa zinaeleza kuwa kwa sasa kumpata kiungo wao Sharaf Shoboub raia wa Sudan ni ngumu jambo lililowafanya waongeze nguvu kwa Francis Kahata na Clatous Chama.

"Kwa sasa ni ngumu kumpata Shiboub ila nguvu kubwa imewekwa kumpata Kahata na Chama ili weweze kujiunga na wachezaji wenzake mazoezi mapema kuanzia sasa ili ligi itakapoanza Juni 13 wawepo.

"Muda wowote wachezaji hawa wawili wanaweza kutua kwani mipango iliyopangwa ni kuona namna gani wanaweza kurejea nchini mapema," ilieleza taarifa hiyo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Patrick Rweyemamu, Meneja wa Simba amesema kuwa mpango wa kuwarejesha wachezaji wote upo.

"Kuna mpango wa kuwarejesha wachezaji wetu wote waliopo nje ila itategemea na hali za nchini kwao zilivyo kwani mipaka ya nchi nyingi bado hazijafunguliwa kutokana na tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona," amesema.

Wachezaji hao waliondoka nchini baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo Machi 17 ili kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic