RELLIANTS Lusajo, mshambuliaji wa Namungo FC amesema kuwa anauwezo wa kucheza timu yoyote ndani ya Bongo kikosi cha kwanza kutokana na uwezo alionao.
"Sina mashaka na uwezo wangu kwa sasa kwani nipo vizuri na nipenda kuwa bora muda wote nina amini janga la Virusi vya Corona likipita nitaendelea kuwa kwenye ubora wangu.
Imekuwa ikielezwa kuwa nyota huyo yupo kwenye hesabu za Yanga pamoja na Simba ambazo zinapasua kichgwa kuipata saini yake.
Akizungumza na Saleh Jembe, Lusajo amesema kuwa hana mashaka na uwezo wake wa kucheza soka la ushindani kutokana na kuamini katika kipaji chake.
"Sina mashaka na uwezo wangu kwa sasa kwani nipo vizuri na nipenda kuwa bora muda wote nina amini janga la Virusi vya Corona likipita nitaendelea kuwa kwenye ubora wangu.
"Kikubwa kwa sasa ni kuendelea kuwa makini na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kwani mambo mengi yamesimama kutokana na janga hili," amesema.
Lusajo ametupia mabao 11 na kutoa pasi tatu za mabao ndani ya Namungo akiwa ni miongoni mwa wazawa wanaofanya vizuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment