ADAM Oseja, mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha Namungo FC kilicho chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery amesema kuwa anafurahia kurejea kwa mechi za ushindani kwa kuwa walikuwa wameukumbuka mpira.
Shughuli za michezo zilisimamishwa tangu Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona ila kwa sasa Serikali imesema kuwa mambo yanaweza kuendelea huku tahadhari ikichukuliwa kuanzia Juni Mosi.
Bodi ya Ligi Ligi Tanzania iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kuwa masuala ya michezo yataanza Juni 13,2020.
Akizungumza na Saleh Jembe, Oseja amesema kuwa muda mrefu walikaa bila kucheza mechi za ushindani jambo lililowafanya waukumbuke mpira.
"Tulikaa muda mrefu bila kucheza ila sababu kubwa ilikuwa ni janga la Virusi vya Corona hatukuwa na namna ya kufanya, kwa kuwa mambo yanarejea tumefurahi tuliukumbuka mpira," amesema.
Oseja alikuwa ni chaguo namba moja wakati ule Namungo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kupanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 amekuwa akisugua benchi huku namba moja akiwa ni Nurdin Barola.
0 COMMENTS:
Post a Comment