May 6, 2020


LIGI Kuu England inatarajiwa Kurejea mwezi Juni itakuwa ikionyeshwa live pia kwenye mtandao wa You Tube baada ya mabosi kukutana na kukubaliana kwamba mambo yote yanapaswa kuwa live.

Ligi mbalimbali duniani zilisimama kwa muda kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia.

Mbali na You Tube ambayo inatajwa kuwa itaonyesha michezo hiyo bure pia vituo vya SkySport na BT Sport navyo vitaendelea kuonyesha michezo hiyo kama kawaida.

Tayari timu za Ligi Kuu England zilianza mazoezi hivi karibuni na msimu unatarajiwa kuendelea Juni 12 huku michezo iliyobaki ili Ligi ikamilike ni 92.

Liverpool iliyo chini ya Jurgen Klopp ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 82 ikiwaacha Manchester City yenye pointi 57 kwa pointi 25 inatakiwa kushinda mechi mbili ili itwae ubingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic