KLABU ya Simba, leo Mei 6, 2020, imeazimisha miaka nane
tangu ilipowanyuka watani zao wa jadi Yanga mabao 5-0.
Simba katika msimu wa 2011/12, iliifunga Yanga mabao 5-0
katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara msimu huo na kutwaa ubingwa chini ya Kocha, Milovan Cirkovic raia wa Serbia.
Katika mchezo huo uliochezwa Mei 6, 2012 kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam, mabao ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi dakika
ya kwanza na 62, Felix Sunzu (dk 53), Juma Kaseja (dk 66) na marehemu Patrick Mafisango
(dk 71).
Kupitia mitandao yao ya kijamii, Klabu ya Simba leo
imeposti taarifa hiyo na kuandika: “Tarehe nzuri kwa Wanasimba, mbaya kwa
mashabiki wa mtani. Historia muhimu (tarehe kama ya leo mwaka 2012).”
Hebu tusisahau zile tarehe Simba alipopigwa 5/5 na Al ahli na motema pembe
ReplyDeletePia tusisahau Yanga tarehe kama hizo Yanga alipigwa 6-0 na Raja casablanca
DeleteHa ha ha ha ha ha ha kiroho kinakuuma brother,na wewe siutaikumbuka tarehe mliyoifunga simba goli moja kupitia kwa morison,mpaka mnashawishi ligi ifutwe mlivyokua na akili finyu,yanga mna shida sana na kwakuwashauri punguzeni mihemko ndugu zangu maisha hayataki pupa mtajikuta mnapoteza kila kitu kwa ujinga wenu.
ReplyDeleteYaliyopita si ndwele tugange yajayo yanafurahisha......yanga mpango mzimaaa utaipenda hata kwakuforce
ReplyDeleteMei 1/1968 yanga ilifanya nini kwa Simba 5-0 Kwahyo Hayo ni matokeo ya uwanjani
ReplyDeleteDaaa hata Leo 25/9/2021 ngao ya jamii mbona hakuna mashabiki kunanani jamanii
ReplyDelete