KUNAPOTOKEA tatizo lolote unaomba msaada na ukija huwezi kuchagua ni yupi anakuletea huo msaada.
Unachotaka wewe ni kulitatua hilo tatizo lako ili maisha mengine yaendelee kama kawaida.
Kuna wakati tunasema si wakati wa kuchagua kitu lazima ukubali na kile kinachotokea kwa wakati ule na hiyo haina namna.
Tumekaa hapa kwa zaidi ya miezi miwili bila kucheza mpira wowote au hata kufanya mazoezi tukalalamika sana kuwa tunakumbuka mpira.
Hali haikuwa nzuri wakati ule kutokana na janga la ugonjwa wa Corona na kweli wote tulikubali na tulipambana.
Sasa hali imeanza kuwa shwali na kwa kuanzia Serikali imerejesha soka lianze kuchezwa kabla ya michezo mingine ili kuweza kuona itakuwaje kabla ya kuanza kwa michezo mingine.
Sasa baada ya Serikali kuruhusu soka lichezwe kwa vituo viwili yaani Dar es salaam na Mwanza tayari watu wameanza kutoa maneno maneno kibao.
Serikali imefanya kama ni msaada tu ili kumalizia msimu huu wa ligi sasa mnataka kuipangia kama mnavyotaka nyie.
Hivi sie Watanzania tunashida gani jamani? Hivi watu mnakosa uelewa na mnataka nini lakini.
Jamani Corona haijaisha kwenye hii nchi ila mmeambiwa hali imeanza kuwa nzuri ndio maana wameanza kuruhusu soka lichezwe.
Sasa watu naona mnataka kuipangia Serikali ifanye mnavyotaka nyinyi nyinyi sio kama inavyotaka yenyewe.
Yaani klabu ya ligi kuu eti inataka kuipangia Serikali ifanye vile inavyotaka kisa ikacheze kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Wengi wanatoa kisingizo cha gharama kubwa kuja kucheza hapa Dar es Salaam sio kweli semeni ukweli unaowakimbiza hapa Dar City.
Gharama za kutembea barabarani kwa safari ndefu kwa basi hazina tofauti kabisa na kukaa hapa Dar es Salaam semeni kuna mipango yenu mnataka kuifanya huko kwenu.
Najua ligi ikichezwa nyumbani na ugenini kuna baadhi ya michezo haitaonyeshwa kwenye Television na hapo sasa kuna kitu lazima kifanyike.
Ligi ikichezwa kwa viwanja vitatu itaonyeshwa kwa Tv najua wengi hicho hawakitaki hata kidogo.
Kingine hakuna mashabiki kuingia viwanjani hata mkicheza huko mikoani hamuwezi hamuwezi kupata pesa jamani.
Tukubali tu tumalize huu msimu na mengine yatafuata msimu ujao maana hili jambo ni la dharula tu sio la kudumu.
Kwenye shida mnatumia njia yeyote ile kutafuta ufumbuzi hivyo lazima tubali kwa hili.
0 COMMENTS:
Post a Comment