Kwa heshima zote napenda kueleza masikitiko yangu juu ya ninachokiona hapo kwenye hiyo VIDEO ya mechi ya Waandishi wa Habari. Hawa ndio waelimishaji wakuu na kioo cha jamii katika mambo mbalimbali, hususani kwa wakati huu jambo muhimu likiwa ni elimu ya afya ya jamii kuhusu njia za kawaida sana na rahisi za kujikinga na ugonjwa wa Virusi vya Korona (COVID-19). Ugonjwa huu bado upo duniani, na hivi karibuni tu nchini Korea Kusini baada ya kuruhusu shule zifunguliwe kwa mafungu, walibaini maambukizi mapya kadhaa ya COVID- 19 ndani ya wiki ya kwanza tu ya shule kufunguliwa. Inasikitisha kuona watu wanaotegemewa kuwa na ufahamu mkubwa wa janga hili, wanaonekana kutokuwa makini na wenye tahadhari. Tazama hakuna hata mmoja wao aliyevaa Barakoa, tazama jinsi walivyosogeleana karibu na hatuna uhakika kama wachezaji walipimwa kwa utaratibu wa uhakika wa kiafya. Kulikuwa na haraka gani ya kufanya hii mechi ambayo haina umuhimu wowote na hivyo kuhatarisha afya za wanaoshiriki hapo na familia zao kule majumbani na wengine wengi wanaoweza kuonana nao baadae? Kuna haja ya kujitathmini hapo na kujirekebisha kwa kuitaarifu jamii kwamba ruhusa iliyotolewa na serikali kuhusu kufanya shughuli za michezo haikumaanisha mambo yafanyike kiholela namna ile. Nawasilisha.
Kaka Saleh Jembe, Heshima yako Mkuu!
ReplyDeleteKwa heshima zote napenda kueleza masikitiko yangu juu ya ninachokiona hapo kwenye hiyo VIDEO ya mechi ya Waandishi wa Habari. Hawa ndio waelimishaji wakuu na kioo cha jamii katika mambo mbalimbali, hususani kwa wakati huu jambo muhimu likiwa ni elimu ya afya ya jamii kuhusu njia za kawaida sana na rahisi za kujikinga na ugonjwa wa Virusi vya Korona (COVID-19). Ugonjwa huu bado upo duniani, na hivi karibuni tu nchini Korea Kusini baada ya kuruhusu shule zifunguliwe kwa mafungu, walibaini maambukizi mapya kadhaa ya COVID- 19 ndani ya wiki ya kwanza tu ya shule kufunguliwa. Inasikitisha kuona watu wanaotegemewa kuwa na ufahamu mkubwa wa janga hili, wanaonekana kutokuwa makini na wenye tahadhari. Tazama hakuna hata mmoja wao aliyevaa Barakoa, tazama jinsi walivyosogeleana karibu na hatuna uhakika kama wachezaji walipimwa kwa utaratibu wa uhakika wa kiafya. Kulikuwa na haraka gani ya kufanya hii mechi ambayo haina umuhimu wowote na hivyo kuhatarisha afya za wanaoshiriki hapo na familia zao kule majumbani na wengine wengi wanaoweza kuonana nao baadae? Kuna haja ya kujitathmini hapo na kujirekebisha kwa kuitaarifu jamii kwamba ruhusa iliyotolewa na serikali kuhusu kufanya shughuli za michezo haikumaanisha mambo yafanyike kiholela namna ile. Nawasilisha.